Baada ya aliyekuwa waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Fredrick Sumaye kudai amepokonywa mashamba yake kwasababu ya kisiasa, hatimaye waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amejibu tuhuma hizo.

Lukuvi amesema kuwa mtu yoyote asiyelipa kodi ya ardhi na kuendeleza ardhi hiyo, ni sababu tosha ya kunyang’anywa ardhi hiyo pamoja na kufutiwa hati ya umiliki kwa kuwa anaingizia hasara serikali.

Waziri Lukuvi amebainisha hayo ikiwa imepita siku moja tokea kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tatu, Fredrick Sumaye kudai chanzo cha kupokonywa shamba lake ni siasa tu za yeye kuhama chama cha CCM na kwenda kuupa nguvu upinzani.

Lukuvi amesema amesema kuwa kila mtu atambue iwe ni kiwanja au shamba kama unatabia ya kutolipa kodi ya ardhi ni sababu tosha ya wewe kunyang’anywa shamba lako au ardhi unayomiliki.

Pia Waziri Lukuvi amesema imekuwa kawaida ya baadhi ya watu wanapowahi maeneo  huwa wanakimbilia kuchukua sehemu zenye manufaa makubwa kwa upande wao na mwishowe wanashindwa kuendelezaa maeneo hayo kama walivyoyakimbilia.

Ikumbukwe kuwa Sumaye ambaye alikuwa waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu ambapo kwasasa ameamia chama cha Chadema amepokonywa mashamba yake ya Mabwepande na Mvomero mkoani Morogoro

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *