Klabu ya Everton imekubali dau la paundi milioni 75 kutoka Manchester United kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji, Romelu Lukaku.

Mchezaji huyo ,mwenye umri ya miaka 24 alikuwa katika orodha ya washambuliaji iliowasilishwa kwa naibu mwenyekiti wa Manchester United Ed Woodward na kocha Jose Mourinho.

Ilidhaniwa kwamba Lukaku ambaye alifunga mabao 25 msimu uliopita angejiunga tena na klabu yake ya zamani Chelsea.

United sasa wanahisi kwamba inawezekana kumpata mshambuliaji huyo wa Ubelgiji baada ya makubaliano hayo.

Klabu hiyo imekuwa katika mazungumzo ya kumsajili Alvaro Morata kutoka Real Madrid lakini wameshindwa kuafikiana hadi sasa.

Pia Manchester United tayari imeanza kuwasiliana na Everton kuhusu mkataba wa aliyekuwa nahodha wa Uingereza Wayne Rooney, ambaye huenda akaondoka Old Trafford na kurudi Goodison Park.

Hatua hiyo inaweza kufanya mazungumzo kuwa rahisi ,hata iwapo kiwango cha fedha kinachozungumziwa kinaweza kuwa juu ya kiwango cha uhamisho wa pauni milioni 89 cha Paul Pogba kujiunga na United.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *