Mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku ameshinda magoli matatu ‘Hat trick’ kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Sunderland iliyofanyika katika uwanja wa Light  jana usiku.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa bila bila lakini kipindi cha pili kilipoanza Everton walionekana kuutawala mchezo huo kwa kushambulia lango la Sunderland kila mara.

Lukaku alitimia dakika 11 kupiga goli zote tatu baada ya kushinda dakika ya 60, 68 na 71 na kuipa ushindi timu yake ya Everton 3-0 dhidi ya Sunderland.

Lukaku: Akiwania mpira na beki wa Sundedrland kwenye ya ligi kuu nchini Uingereza jana usiku ambapo Everton imeshinda 3-0.
Lukaku: Akiwania mpira na beki wa Sundedrland kwenye ya ligi kuu nchini Uingereza jana usiku ambapo Everton imeshinda 3-0.

Sunderland inayonolewa na kocha David Moyes imeonekana kuanza vibaya kwenye mechi za ligi kuu msimu huuu baada ya kufungwa mechi tatu na kusuluhu mechi moja.

Kwa matokeo hayo inaiweka Sunderland katika nafasi mbaya ya kushuka daraja msimu huu kutokana na timu yake kutomkuwa kwenye kiwango licha ya kusajili baadhi ya wachezaji wapya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *