Mshambuliaji wa klabu ya Everton, Romelu Lukaku amekataa kusaini mkataba na timu hiyo.

Klabu ya Everton ilikuwa na matumaini kwamba mchezaji huyo raia wa Ubelgiji ataongeza mkataba mwingine wa miaka mitano inayoaminika kugharimu pauni 140,000 kwa wiki.

Agenti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, Mino Raiola amesema kuwa mteja wake alikuwa na uwezekano wa asilimia 99.9 kusaini mkataba mpya katika timu hiyo.

Lakini Lukaku ameiambia klabu hiyo kwamba hana mpango wa kuongeza mkataba mpya ambao umesalia miaka miwili kumalizika.

Lukaku hajaficha kuhusu mpango wake wa kutaka kusakata dimba la vilabu bingwa Ulaya na amehusishwa na uhamisho wa kurudi katika klabu yake ya zamani Chelsea, ambapo alijiunga na Everton kwa kitita cha pauni milioni 28 mwaka 2014.

Ombi la mkataba wa Everton bado lipo wazi huku klabu hiyo ikisema kuwa majadiliano zaidi huenda yakapata makubaliano.

Lukaku hajakubali mkataba wowote na Everton huenda ikaitisha kitita cha pauni milioni 60 kwa mchezaji huyo aliyefunga mabao 19 msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *