Kocha wa Barcelona, Luis Enrique ametangaza kuwa ataachana na mabingwa hao wa Uhispania mwisho wa msimu huu.

Enrique atakuwa amehudumu kama meneja wa klabu hiyo kwa misimu mitatu na kushinda mataji kadhaa likiwemo ligi mabingwa Ulaya.

Toka ajiunge na klabu hiyo Enrique ameshinda kombe la vilabu bingwa na mataji mengine mawili alipojiunga na Barcelona na kuwasaidia kushinda makombe 2 mwaka uliopita.

Lakini licha ya klabu hiyo kuongoza ligi ligi Barcelona iko katika hatari ya kutoka katika kombe la kilabu bingwa Ulaya msimu huu baada ya kufungwa 4-0 na Prais St-Germain.

Enrique amesema kuwa sababu kuu ya yeye kutaka kujiuzulu ni kwamba anahitaji kupumzika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *