Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kujifunza uzoefu wa utendaji wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) ili kuimarisha utawala bora nchini.

Jaji mstaafu Lubuva ametoa mwito huo wakati akieleza uzoefu wake juu ya utendaji kazi wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya tume hiyo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Amesema pamoja na TKU kukabiliwa na changamoto nyingi wakati inatekeleza majukumu yake wakati huo, lakini ilifanya kazi zake kwa ufanisi kutokana na malalamiko ya wananchi yaliyoshughulikiwa kwa wakati huo.

Ameongeza kuwa itakuwa si kusifia kusema kuwa TKU ilifanya kazi nzuri katika kipindi chake cha miaka 32 kwani ulikuwa wakati ambao Tanzania ndio ilikuwa imejikomboa kutoka utawala wa Kikoloni na ilijitahidi kuendesha shughuli za maendeleo kwa wananchi.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa walithubutu kwa mwalimu kuleta wazo la kuanzisha TKU ili kunusuru wananchi kutokana na madhila ya matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi na watendaji kwa wakati huo.

Katika maadhimisho hayo, Mwalimu Nyerere na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi walipata Tuzo na Cheti cha kutambua mchango wao kuweka misingi ya uwajibika na utawala Bora.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *