Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ Edward Lowassa na viongozi wengine wa chama hicho amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita leo Januari 16, 2017.

Lowassa na wenzake walikamatwa katika kituo cha mabasi cha zamani cha Geita wakitokea mkoani Kagera kwenye ziara kuelekea kwenye kampeni za uchaguzi Kata ya Nkome.

Baada ya kusimamishwa na wananchi hao waliokuwepo eneo hilo, baada ya kushuka kwenye gari kwa ajili ya kusalimiana nao ndipo polisi waliwakamata na kuwampeleka Kituo Kikuu cha Polisi Geita.

Chanzo: Global Publishers

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *