Aliyekuwa mgombea urais kupitia umoja wa UKAWA, Edward Lowassa na mwanachama mwenzake wa CHADEMA, Fredrick Sumaye jana walimtembelea Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema katika Gereza Kuu la Kisongo jijini Arusha.

Lowassa aliongozana na Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ambaye pia ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha.

Calist alisema Lowassa alifika gerezani hapo saa tano asubuhi huku Sumaye aliyeongozana na Naibu Meya wa Arusha, Viola Lazaro akifika baadaye saa saba mchana.

Calist alisema Lowassa akizungumza na Lema, alimwambia kuwa mahakama ndiyo chombo pekee kinachoaminiwa na wananchi, hivyo kinapaswa kutenda haki kwa watu wote.

Alisema Lowassa aliridhishwa na afya ya Lema na kumtaka awe mvumilivu, hasa katika kipindi hiki anachokabiliwa na kesi na aliwataka wananchi wa Arusha Mjini kumwombea kiongozi huyo.

 

Kwa upande wake, Sumaye alisema kuwa alimtaka mbunge huyo kuwa jasiri katika kipindi hiki kwa sababu suala linalomkabili litafika mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *