Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa na Frederick Sumaye wanatarajia kufanya ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Viktoria na Serengeti.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imesema  ziara hiyo ina lengo la kukiimarisha chama katika ngazi za chini kupitia mikutano ya ndani.

Sumaye na Lowassa wanatarajiwa kuhutubia mikutano ya hadhara katika baadhi ya kata ambazo zinarudia uchaguzi kwa nafasi za udiwani katika kanda hizo kadiri ya ratiba ilivyopangwa.

Pia amesema Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe  na wajumbe wa Kamati Kuu, wataongoza timu mbalimbali zitakazofika kwenye majimbo yote ya kanda hizo hadi Januari 20.

Viongozi wakuu wengine watakaongoza timu mbalimbali ni pamoja na Makamu Mwenyekiti (Bara), Profesa Abdallah Safari na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Said Issa Mohamed.

Wengine ni Katibu Mkuu, Dk. Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu (Tanganyika), John Mnyika na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalim Juma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *