Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amemtembelea kumjulia hali mbunge Singida, Tundu Lissu ambaye anaendelea kupatiwa matibu Nairobi nchini Kenya.

Lowassa ameongozana mke wake Mama Regina Lowassa ambapo leo hii walifika hospitalini hapo kumjulia hali Mhe. Lissu.

Tangu picha za Lissu kuanza kuonakana pindi watu wanapoenda kumjulia hali, viongozi wa juu na wabunge wamekuwa wakifanya hivyo.

Miongoni mwao ni mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, Mhe. John Heche na mbuge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi ambao hivi karibuni wameonekana wakiwa katika picha ya pamoja.

Tundu Lissu alipigwa risasi akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma na watu wasiujulikana na sasa anaendelea vizuri katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *