Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema kuwa Chedema itashinda uchaguzi wa mwaka 2020 kutokana na hali ilivyo na inavyoendelea nchini.

Lowasa ameyasema hayo wakati akifungua semina kwa wabunge, mameya na madiwani wa chama hicho wa Jiji la Dar es Salaam ikilenga kujadili kazi waliyofanya ya kutumikia wananchi.

Pia amesema Chadema itapita maeneo ambayo watu wako nyuma kielimu ili kuwaelewesha nia njema ya kuwaletea maendeleo na kuwapa elimu.

Vile vile Lowassa amewataka mameya na viongozi wengine wa Chadema jijini humo kukataa kutoa mikataba ya aina yoyote kienyeji na kushughulikia suala la maegesho, ili isifike mahali wananchi wakajuta kuichagua Chadema na kusema afadhali CCM.

Kauli hiyo ya Lowassa inakuja kufuatia kilio kikubwa cha wananchi wanaolia kukabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi, huku wengi wakidhani imesababishwa na kubana matumizi kunakofanywa na Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *