Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Edward Lowassa amewasili makao makuu ya Jeshi la Polisi kwenye ofisi za Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.

Lowassa amewasili leo majira ya saa mbili asubuhi huku akiambatana na mkewe, Regina na mwanasheria wake, Peter Kibatala.

Hii ni mara ya nne kwa Lowassa kuripoti hapo akituhumiwa kutoa kauli za kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa  Juni 23, na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa gerezani  akidai utaratibu wa kisheria ufanyike ili waachiwe huru.

Polisi wameimarisha ulinzi eneo hilo, huku Lowassa akiwa ndani tayari kwa kuhojiwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *