Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa amewasili makao makuu ya Polisi kwa ajili ya mahojiano na mkurugenzi wa upelelezi na makosa ya jinai DCI, Robert Boaz.

Lowassa amewasili leo majira ya saa tatu akiwa ameambatana na wakili wake, Peter Kibatara ambao wamewasili kwa msafara wa magari matatu.

Ulinzi uliimarishwa makao makuu hayo kama ilivyokuwa siku ya kwanza kuwasili maeneo hayo kwa mara ya kwanza.

Hii ni mara ya tatu kwa Lowassa kuwasili makao makuu hayo ya Polisi akikabiliwa na kesi ya uchochezi .

Wakili wake Peter Kibatala amesema kuwa Lowassa ametakiwa kurudi tena makao makuu hayo Alhamis ijayo kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *