Aliyekuwa mgombea urais kupitia UKAWA na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema kuwa hakuhudhuria misiba ya aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta na waziri wa Elimu wa zamani, Joseph Mungai kwasababu alikuwa anamuuguza mdogo wake Afrika Kusini.

Lowassa amesema kuwa hakuweza kuhudhuria misiba hiyo kwakuwa alikuwa nchini Afrika Kusini akimuuguza mdogo wake anayeitwa Bahati Lowassa na si vinginevyo.

Lowassa amesema kuwa “Mdogo wangu Bahati Lowassa ni ofisa ubalozi nchini Afrika Kusini, alikuwa anaumwa na alikuwa amelazwa. Kwa siku zote nilikuwa huko kumuangalia. Nisingeacha kuhudhuria misiba hiyo,”.

Pia Lowassa ameongeza kwa kusema kuwa alikuwa pamoja na waombolezaji kwa kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sitta kupitia vyombo vya habari pamoja na kumtumia mwanasheria wake kuwasilisha salamu zake za rambirambi kwa familia ya Mungai.

Samuel Sitta alifariki Novemba 7 mwaka huu nchini Ujerumani alipokuwa ameenda kutibiwa maradhi ya tezi dume ambapo siku iliyofuata alifariki joseph Mungai.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *