Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema kuwa anatarajia kugombea tena urais kupitia Chadema katika uchaguzi wa urais mwaka 2020.

Lowassa amesema kuwa licha ya changamoto nyingi anazokutana nazo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lakini adhima yake ya kugombea urais mwaka 2020 ipo pale pale.

Lowassa ambaye ni waziri mkuu mstaafu amethibitisha hayo wakati akifanya mahojiano na maalumu na waandishi wa Nation Media Group jijini Nairobi nchini Kenya ambapo alihudhuria mazishi ya waziri wa Usalama nchini humo.

Lowassa amesema kuwa “Kwa mapenzi ya Mungu nitajaribu tena mwaka 2020 na nitapita kwa mikono safi.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa Wafuasi wangu walitaka tuingie mitaani kudai ushindi, lakini kulikuwa na bunduki nyingi mikononi mwa wanajeshi. Niliogopeshwa na umwagikaji wa damu. Sikutaka kuingia Ikulu kupitia damu za watu kwa sababu sistahili hivyo,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *