Aliyekuwa mgombea urais kupitia Ukawa kwenye uchaguzi mkuu na mjumbe wa Kamati kuu Chadema, Edward Lowassa amesema njia ya kuingia Ikulu 2020 ni nyeupe katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huo huku akitaka wananchi kujitokeza kupiga kura.

Lowassa ameyasema hayo Kahama mkoani Shinyanga, kijiji cha Mseki nyumbani kwa Kada wa Chadema, James Lambeli.

Kiongozi huyo amesema anashindwa kuongea na wananchi wa kijiji hicho kwa kuhofia kukamatwa na polisi kama alivyofanyiwa Geita na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu mpaka itakapofika 2020.

Lowassa amewataka wananchi kuwa wavumilivu hadi itakapofika 2020 huku akiwataka wajitokeze kupiga kura kama atakuwa hai atagombea tena urais kupitia muungano wa vyama pinzani UKAWA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *