Mjumbe wa halmashauri kuu ya Chadema, Edward Lowassa leo amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, anayetibiwa jijini Nairobi baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mjini Dodoma wiki iliyopita.

Ujumbe wa Lowassa ambao ameuweka kwenye mtandao wa Twitter unasema kuwa Earlier today i paid a visit at Nairobi Hospital to see our MP, President of TLS and dear friend Tundu Lissu.

Kwa kiswahili alimaanisha kuwa ‘Mapema leo nilikwenda Hospitali ya Nairobi kumwona Mbunge na Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) ambaye ni rafiki yangu mkubwa’.

Lissu alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa risasi na watu ambao hawajulikani alipokuwa anarejea nyumbani kwake mchana baada ya kikao bungeni ambapo alikimbizwa Hospitali ya Dodoma na hatimaye Nairobi kwa matibabu zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *