Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Edward Lowassa amehudhuria mahakamani kusikiliza uamuzi wa Mahakama kuhusu dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema unaotolewa leo.

Mbali na Lowassa vingozi wengine wa Chama hicho waliohudhuria Mahakamani hapo ni ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vicent Mashinji, Waziri Mkuu Msaatafu Sumaye na Meya wa Jiji la Arusha Mjini Kalisti Lazaro.

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo inatarajiwa kusikiliza maombi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambaye ameendelea kusota rumande kwa miezi minne.

Lema amekamatwa tangu Novemba 2 mwaka jana akiwa bungeni Dodoma, amewekwa mahabusu katika Gereza la Kisongo, Arusha.

Jaji Salma Magimbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ndiye atakayesikiliza rufaa hiyo namba 126 ya mwaka jana ambayo iliwasilishwa na mawakili wanaomtetea, Kibatala, John Mallya na Sheck Mfinanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *