Aliyekuwa mgombea uras kupitia UKAWA na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amesema anamshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kuruhusu vikao vya ndani.

Hayo aliyasema Dar es Salaam alipofungua mafunzo ya siku mbili kwa madiwani, wabunge na viongozi wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam yanayoendelea kutolewa na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani ambapo mjumbe huyo alisifia vikao hivyo.

Akizungumzia ziara za kanda zilizofanywa na viongozi wa chama hicho hivi karibuni, Lowassa alisema vikao vya ndani vimewapa nafasi na muda mwingi wa kuzungumza na wanachama kwa karibu zaidi.

“Tumefanya ziara, tumeona hali ya barabara ni nzuri lakini hali ni nzuri zaidi tulivyozungumza na wanachama wetu na tunamshukuru Rais aliona hakuna haja ya mikutano ya nje akatupatia vikao vya ndani, ni vizuri, ni vitamu zaidi kuliko vile vya nje,” alisema Lowassa.

“Tunapata nafasi nzuri ya kuzungumza na wanachama ana kwa ana, kwa muda mrefu kwa mapenzi na mahaba, Nataka niwaambie Chadema ipo imara sana, watu walidhani wamekata tamaa lakini wapo imara katika kuhakikisha chama kinapata ushindi mwaka 2020.”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *