Mwanamuziki wa Bongo fleva, Barakah The Prince kupitia lebo yake mpya ya BANA amemsajili mwanamuziki mkongwe wa hip hop nchini Lord Eyez atakayesimamiwa chini ya lebo hiyo.

Muimbaji huyo amedai kuwa Lord Eyez ataungana na mpenzi wake, Naj kama wasanii wa label hiyo na kwamba hivi karibuni nyimbo zao zitatoka kupitia chini ya lebo hiyo.

Pia amesema kuwa lengo la kumchukua Lord Eyez ni kutokana na kukubali uwezo wake na kwamba kutokana na kutumbuiza naye kwenye show kadhaa, amegundua kuwa ana mashabiki kibao.

Lord Eyez alikuwa kwenye kundi la Weusi alisimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu ndani ya kundi hilo maarufu nchini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *