Klabu ya Leicester City imefanikiwa kuwatoa Liverpool kwenye Kombe la Carabao baada ya kuwafunga 2-0 kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa King Power.

Mabao hayo yalipatikana baada ya Liverpool kutawala kipindi cha kwanza ambapo Philippe Coutinho alikuwa amecheza vyema sana kabla ya kutolewa uwanjani.

Alex Oxlade-Chamberlain na Dominic Solanke walionunuliwa na Liverpool majuzi wote walipoteza nafasi nzuri za kufunga.

Kwingineko Roy Hodgson alipata ushindi wake wa kwanza Crystal Palace wakiwa nyumbani dhidi ya Huddersfield.

Tottenham nao walichukua dakika 65 kuwapangua Barnsley uwanjani Wembley nao Leeds wakawalaza Burnley kwa mikwaju ya penalti uwanjani Turf Moor.

Liverpool watasafiri tena Leicester kwa mechi ya Ligi ya Premia siku ya Jumamosi, mechi ambayo itaanza saa moja unusu jioni saa za Afrika Mashariki.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *