Klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza imekubaliana na Newcastle United kwa ajili ya kumsajili kiungo, Georginio Wijnaldum kwa ada ya paundi milioni 25.

Kiungo huyo mwenye miaka 25 raia wa Uholanzi amecheza mechi 30 za kimataifa hapo jana alipimwa afya katika uwanja wa mazoezi wa Liverpool, Melwood na leo Ijumaa atamalizia taratibu za mwisho za kijiunga na timu hiyo

Klabu hiyo ya Liverpool yenye maskani yake Anfield itamsainisha miaka mitano kiungo huyo akikamilisha taratibu zote.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Kloop anamsajili mchezaji huyo ili kuimalisha kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza unaotarajiwa kuanza mwezi Agosti mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *