Goli moja kutoka kwa Mane na lingine kutoka kwa Countinho yametosha kuipa Liverpool alama tatu muhimu baada ya kuifunga West Bromwich goli 2-1 kwenye mechi ya ligi kuu iliyofanyika katika uwanja wa Anfield.

Mane ndiyo alikuwa wa kwanza kuipatia timu hiyo goli la kuongoza katika dakika ya 20 huku goli la pili likifungwa na Coutinho dakika ya 35 mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Liverpool ilikuwa mbele kwa goli hizo.

Goli la kufutia machozi la West Browich limefungwa na McAuley katika ya 81 ya mchezo na kufanya matokeo kumalizika 2-1.

Kwa matokeo hayo Liverpool imefikisha jumla ya alama 20 baada ya kucheza mechi 9 hadi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *