Livepool imeifunga Arsenal 3-1 kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza iliyofanyika katika uwanja wa Anfield.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Liverpool walikuwa mbele kwa goli 2-0 ambapo magoli yao yalifungwa na Firmino dakika 9 na goli la pili likifungwa na Saido Mane katika 40 ya mchezo huo.

Goli la tatu limefungwa na Georginio Wijnaldum katika dakika ya 90 ya mchezo huo baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Orig huku goli la kufutia machozi la Arsenal likifungwa na Danny Welbeck dakika ya 57.

Kutokana na matokeo hayo Liverpool imepanda mpaka nafasi ya tatu baada ya kufikisha alama 52 akiwa nyumba ya Chelsea na Tottoenham.

Ligi hiyo inaendelea tena kesho kwa michezo miwili ambapo Tottenhama anacheza na Everton katika uwanja wa White At Lane na Sunderland wakiikaribisha Manchester City katika uwanja wa Stadium of Light.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *