Liverpool leo inaikaribisha Chelsea kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza itakayofanyika katika uwanja wa Anfield.

Timu hizo zinakutana mara ya pili kwenye ligi ya kuu nchini Uingereza msimu huu ambapo kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika katika uwanja wa Stanford Bridge Liverpool ilishinda 2-1.

Chelsea wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 55 huku Liverpool akiwa na nafasi ya 4 akiwa na alama 45 baada ya wote kucheza mechi 22 kila mmoja.

Timu hizo zimekutana mara 165 liverpool imeshinda mara 71 na Chelsea imeshinda mara 56 huku wakitoka suluhu mara 38.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *