Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya nchini imekamata kiasi cha lita 4,694 za kemikali zinazoweza kutengeneza dawa za kulevya.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Mamlaka hiyo, Rogers Sianga leo jijini Dar es Salaam baada ya kukamatwa kwa kemikali hizo.
Sianga amesema kuwa kemikali hizo zimekamatwa baada ya kufanyika oparesheni maalum iliyofanyika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Sianga amesema kemikali hiyo imekamatwa katika Mtaa wa Kipepeo eneo la Mwenge jijini Jijini Dar es Salaam.
Pia amesema pia wamebaini kuwepo kwa maghala mengine yaliyopo Bagamoyo mkoani Pwani na Moshi mkoani Kilimanjaro ambayo yanatengeneza kemikali hizo za madawa ya kulevya.
Kamishna Sianga amesema kuwa operesheni hiyo bado inaendelea mpaka kuhakikisha janga hilo la madawa ya kulevya yanamalizika nchini.