Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Lipumba amesema kuwa kuwa anaunga mkono suala la watuhumiwa wa madawa ya kulevya.

Lipumba amesema kuwa anaisapoti serikali kuhusu suala la watuhumiwa wa madawa ya kulevya, kukamatwa na kuongeza kuwa serikali inapaswa kuungwa mkono katika suala hilo.

Pia ametoa ushauri kwa Serikali kuwa isiwapeleka watu mahakamani bila kuwa na ushahidi wa kutosha kwani suala hilo litaigharimu fedha nyingi katika kuendesha kesi hizo.

Mwenyekiti huyo amesema hayo katika viwanja vya mahakama alipokwenda kusikiliza kesi baina yake na maalim Seif Sharif Hamad.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *