Mwanamuziki wa Bongo fleva, Sunday Mjeda ‘Linex’ amesema kuwa anatarajia kufanya kolabo na staa wa muziki kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone hivi karibuni.

Linex amesema tayari ameshamtumia Jose Chameleone beat ya nyimbo hiyo kwa ajili ya maandalizi ya wimbo huo mpya.

Mwanamuziki huyo amesema kwamba kwa upande wake ameshaingiza verse, bado Jose lakini na ataingiza Jumatatu hii kwa sababu alishamtumia beat.

Linex ameongeza kwa kusema nyimbo hiyo itakuwa kazi ambayo itakuja kukamilika lakini bado  kwa sababu kuna mambo mengi yanakuja kutoka kwake hivi karibuni kabla ya kutoka kwa nyimbo hiyo.

Jose Chameleone
Jose Chameleone

Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wake kuendelea kusubiria video ya wimbo ‘Hewala’ aliomshirikisha Christian Bella.

Linex ni miongoni mwa wasanii wenye vipaji vya hali ya juu ya uimbaji kutokana na nyimbo zake kugusa nyoyo za watu pamoja na sauti yake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *