Linah awataka wasanii wa kike kuacha majigambo

0
46


Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga amewataka wasanii wenzake wa kike waonyeshe ushirikiano na waache tabia za kujiona bora kuliko wenzao.

Linah ametoa ya moyoni kwa wasanii wenzake Wakike waache majigambo na kujisifia ovyo baada ya kufanyakazi ili wafike mbali ki muziki.

Mwanamuziki huyo amewataka wasanii wenzake wa kike wafanye kazi waache tabia ya kujigamba kwani haiwasaidii kitu badala yake inawarudisha nyuma kimuziki kwani wanashindwa kusaidiana kutokana na majigambo hayo.

Kauli hiyo ya Linah inahusishwa na alichoandika mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu kuwa hakuna wasanii wa kike wa kushindwanisha naye badala yake ashindanishwe na wasanii wa kiume.

LEAVE A REPLY