Mwanaumuziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga amekiri kutoa mimba takribani mbili kabla ya hii aliyonayo sasa hivi na anategemea kujifungua hivi karibu.

Linah amesema anajutia hilo na sababu iliyompelekea kutoa mimba hizo ni kwa sababu alikuwa anamuhofia baba yake kwakuwa hakuwa ameolewa na kudai baba yake alisha watahadharisha juu ya kubeba mimba wakiwa nje ya ndoa wajitenge wenyewe kwenye familia yao.

Licha ya kukiri kutoa mimba hizo mbili lakini Linah ameshindwa kuweka hadharani waliokuwa wanahusika na mimba hizo kabla ya kutoa.

Mwanamuziki huyo kwasasa anaujauzito alioupata kutoka kwa mpenzi wake ambaye wanatarajia kufunga ndoa siku za baadae.

Linah ameungana na muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel ambaye pia alikiri kutoa mimba kipindi cha nyuma kabla ya kuzaa na dansa wa Diamond, Mose Iyobo.

Utoaji mimba imekuwa kawaida kwa mastaa nchini na duniani kwa ujumla kutokana na kukabiliwa na ujana na kutokuwa tayari kuzaaa wakati huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *