Mwananmuziki maarufu nchini Marekani, Lil Wayne ametangaza kustaafu muziki anaofanya kwasasa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter mwanamuziki huyo aliandika: “Sasa sijiwezi tena, haka kiakili, na naondoka kwa staha na nashukuru mashabiki wangu.”

Hata hivyo hajafafanua iwapo ataacha kabisa uimbaji wa muziki au ataacha tu uimbaji wa muziki wa kufoka.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 33 hata hivyo amesema hataki kuonewa huruma kutokana na uamuzi huo.

Lil Wayne amekuwa akigonga vichwa vya habari hivi karibuni kwa visa mbalimbali kutokana na tabia zake.

Amekuwa na mzozo wa muda mrefu na Cash Money Records kuhusu kucheleweshwa kwa albamu yake ya 11 ambayo imepewa jina Tha Carter V.

Pia Lil Wayne alishutumu kampuni hiyo siku mbili zilizopita akitumbuiza na Drake mjini Miami nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *