Ligi kuu soka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imesitishwa kwa muda usiojulikana kutokana na sababu za kiusalama.

Serikali ililitaka shirikisho la soka nchini humo kusitisha mechi za ligi kuanzia leo kutokana na sababu za kisalama.

Sababu ya kusitishwa kwa ligi hiyo ni kutokana na wasiwasi uhenda kukatokea vurugu kwasababu uongozi wa Rais Joseph Kabila utafikia kikomo wiki ijayo.

Katika baadhi ya mechi ya ligi hiyo mashabiki walisikika wakiimba kwamba muhula wa Kabila unamalizika wiki ijayo.

Kabila anatakiwa kung’atuka 19 Desemba lakini amesema anapanga kusalia madarakani hadi Aprili 2018, wakati ambao serikali imesema itaweza kufanya uchaguzi ambao ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *