Ligi kuu nchini Uingereza kesho itaendelea tena katika viwanja saba tofauti ikiwa ni mechi za pili toka kuanza kwa ligi hiyo.

Klabu ya Swansea itaikaribisha Manchester Utd katika uwanja wa Liberty Stadium katika kisiwa cha Wales.

Huku Bournemouth ikiwa mwenyeji wa Watford katika mechi itakayofanyika saa 11:30 kwa masaa ya Afrika Mashariki.

West Brom itasafiri kuwafuata Bunley katika mechi hiyo itakayokuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu hizo.

Baada ya mechi ya kwanza kuambulia points 1 klabu ya Liverpool itaikaribisha  Crystal Palace katika uwanja wa Anfield huku mechi hiyo ikiwa na upinzani mkubwa kutokana na timu hizo kuwa wapinzani wanapokutana.

Kwa upande wa Southampton wenyewe watakuwa nyumbani katika uwanja wa St. Marry wakiwavaa West Ham United ambaye alifungwa goli nne na Manchester United wiki iliyopita.

Stoke wao watakuwa nyumbani katika uwanja wa Britania Studium wakiwakaribisha Arsenal kutoka London.

Leicester City baada ya kufungwa dhidi ya Arsenal wiki iliyopita sasa watakuwa nyumbani King Power kucheza dhidi ya Brighton iliyopanda daraja msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *