Shirikisho la soka nchini TFF limesema kuwa uwanja wa Uhuru maarufu kama shamba la bibi utaanza kutumiwa kwa mechi za ligi kuu Tanzania bara na ligi daraja la kwanza msimu huu baada ya kukamilika.

Ofisa Habari wa Shirikisho hilo,  Alfred Lucas amesema kwamba mechi ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo itakuwa kati ya Simba SC na Ruvu Shooting ya pwani.

Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki kupisha mechi za mwisho za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, washindi wa Ngao ya Jamii, Azam FC watakuwa wageni wa Prisons wakati Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam,

Washindi wa tatu wa Ligi Kuu msimu uliopita, Simba SC watamenyana na Ruvu Shooting na Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara mabingwa watetezi, Yanga SC watakuwa wageni wa Ndanda FC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *