Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel ameingiza sokoni filamu mpya inayokwenda kwa jina la ‘Christmas Eve’ ambayo imetoka siku chache zilizopita.

Licha ya soko la filamu kushuka kwasasa nchini lakini muigizaji huyo ameamua kuwapa raha mashabiki wake ambao walimmisi kwa muda mrefu kutokana na kukaa kimya katika suala zima la uigizaji.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Aunty Ezekiel ameandika ujumbe wa kuwafahamisha mashabiki wake kama filamu hiyo sasa ipo sokoni wanaweza kuipata katika maduka yote ya filamu hapa nchini.

Alichokiandika Aunty Ezekiel kupitia akaunti yake ya Instagram “Usiamini kila kitu unachokiona au kusikia….. Kwasababu kila hadithi Ina pande Tatu yao, yako, Na ukweli,….. Christmas eve bonge LA movie iko mtaanii now …. Go get ur og copy,”.

Mbali na Aunty Ezekiel aliyeigiza filamu hiyo wengine ambao wameonesha vipaji vyao katika filamu hiyo ni Husna Iddy, Lissa Tarimo, Vivian Minja na Prince HDV ambaye ameigiza filamu mbali mbali nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *