Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) leo amerejeshwa tena rumande kwa mara nyingine baada ya kukosa dhamana kwa mara ya tatu mfululizo.

Ombi hilo la dhamana lilikuwa la tatu kwa mbunge huyo tangu alipoingizwa mahabusu Novemba 3 mwaka huu.

Mahakama mkoani Arusha imekataa ombi la kurejea kesi hiyo na kushauri mawakili kupinga zuio la dhamana.

Lema anakabiliwa na tuhuma ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, ombi hilo la dhamana linakuwa la tatu baada ya kukwama mara mbili tangu alipoingizwa mahabusu.

Lema ambaye anatetewa na mawakili sita, Peter Kibatala, John Mallya, Charles Adiel, Adam Jabir, Faraja Mangula na Sheck Mfinanga, dhamana yake licha ya kutolewa na Hakimu Mkazi, Desdery Kamugisha ilipingwa kutokana na notisi ya rufani iliyowasilishwa na mawakili wa Serikali.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *