Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amemwomba Rais Dk. John Magufuli kuunda tume ya uchunguzi au avunje halmashauri ya jiji la Arusha.

Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya hivi karibuni kikao cha Baraza la Madiwani katika Jiji la Arusha kupitisha azimio la kodi za vibanda vilivyojengwa stendi ndogo mjini Arusha kutakiwa kulipia halmashauri moja kwa moja na si kupitia madalali.

Lema amesema kwa muda mrefu kumekuwa na hali ya kutoheshimiwa kwa maazimio yanayotolewa na Baraza la Madiwani jambo ambalo halileti picha nzuri kwa jamii.

Amesema jiji liliingia mkataba wa miaka 10 na waliojenga vibanda hivyo tangu mwaka 1994 na baada ya hapo vitarudi chini ya umiliki wa halmashauri ya jiji lakini tangu wakati huo hadi sasa kumekuwa na kutoelewana na Serikali imekuwa ikikosa mapato yake.

Mbunge amedai kwamba wapo baadhi ya viongozi wa Serikali wamekuwa wakiandaa mikakati kwa kushirikiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  yenye lengo la kudhofisha maeneo yanaongozwa na wapinzani.

Amesema suala la malipo hayo awali wafanyabiashara walikubaliana na uamuzi wa jiji lakini baada ya kuteuliwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Arusha ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa, Mrisho Gambo aliingia suala hilo na kumpa maagizo kwa kuwakingia kifua watu waliojenga vibanda hivyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *