Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji Polisi kumshikilia mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent Academy baada ya trafiki waliokuwepo barabarani wakati wa ajali iyouwa watu 35 mkoani Arusha.

Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu Jambo hilo, Lema amesema kuwa katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona basi hilo kama limezidisha watoto na hawakuvaa mikanda.

Lema amesema kuwa badala ya kukamatwa kwa trafiki hao wanamkamata mmiliki wa shule wakati hakuwepo.

Akijibu hoja hiyo, Naibu Spika, Tulia Ackson amesema kuwa suala hilo halikutokea bungeni kwa hiyo halina jibu.

Jana Jeshi la polisi mkoani Arusha limesema kuwa linamshikilia mmiliki wa Shule hiyo baada kuruhusu basi kupakiza idadi kubwa ya wanafunzi ambapo lilitakiwa kubeba watu 30 badala yake likabeba watu 38.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *