Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema  amehimiza ushirikiano wa wapinzani kuwa kitu kimoja na kudai utawala bora.

Lema amesema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kumbizi ya miaka 50 ya Azimio la Arusha, huku akisema huu ni wakati wa vyama vya upinzani kushirikiana.

Mbunge huyo amesema amehudhuria mkutano huo kutokana na kampeni ya ushirikiano wa vyama vyote vya upinzani waliokubaliana kupinga mwenendo wa Serikali.

 “Mkiwa na mkutano semeni niwaalike na wanachama wa Chadema waje wawape ushirikiano, lengo letu ni kuhakikisha haki inatendeka bila matabaka ya walionacho na wasionacho wala makabila,”.

Katika mkutano huo, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amezungumzia ukwepaji kodi unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa na kusema kuna idadi kubwa ya kampuni za uwekezaji ambazo zinafanya hivyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *