Kesi ya Mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema (Chadema) ambaye anatuhumiwa kwa uchochezi imeendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambapo Lema amerudishwa rumande baada ya upande wa Jamhuri kutoa hoja za kukata rufaa iliyopelekea Lema kukosa dhamana.

Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Desdery Kamugisha alikuwa amefikia hatua ya kutoa dhamana lakini upande wa Jamhuri ulileta hoja hiyo ambapo Hakimu alikubaliana na kusitisha dhamana hiyo hadi pale upande wa Jamhuri utakapokata rufaa

Wakili wa CHADEMA, Shedrack Mfinanga amesema baada ya hakimu kutoa uamuzi huo wataendelea kusubiri na kufuatilia ili waweze kuamua kuhusiana na hatua watakazochukua juu ya rufaa hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *