Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amewataka mawakili wake kutokukata rufaa tena huku akiwaeleza kuwa, kwa sasa yupo tayari kuendelea kukaa rumande hadi pale atakapoachiliwa huru.

Lema anashikiliwa katika mahabusu ya Magereza ya Kisongo mjini Arusha, anakabiliwa na tuhuma ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

Kauli hiyo ya Lema ameitoa leo kufuatia Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kukataa kusikiliza rufaa yake ya maombi ya dhamana.

Ombi hilo la dhamana lilikuwa la nne baada ya kukwama mara tatu tangu alipoingizwa mahabusu.

                                                                                           

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *