Leicester City wamefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani baada ya kuifunga Sevilla magoli 2-0 kwenye mechi ilyofanyika katika uwanja wa King Power.

Baada ya matokeo hayo Leicester City imefuzu kwa jumla ya magoli 3-2 baada ya mechi ya kwanza kufungwa 2-1.

Goli la kwanza limefungwa na nahodha wa Leicester Wes Morgan katika dakika ya 27, na kufanya matokeo kuwa ya sare ya 2-2 dhidi ya Sevilla ambao walionekana kutocheza kwa kuelewana.

Marc Albrighton alifunga goli muhimu la pili mapema katika kipindi cha pili, kabla ya kiungo Samir Nasri kuoneshwa kadi ya pili ya manjano na kutolewa nje.

Licha ya kucheza pungufu, Sevilla walipoteza nafasi ya kuupeleka mchezo katika muda wa ziada baada ya Kasper Schmeichel kuokoa mkwaju wa penati uliopigwa na Steven Nzonzi.

Katika mchezo mwingine, Juventus walitinga robo fainali ya michuano hiyo kwa kuilaza Porto bao 1-0 .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *