Mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Cleveland Cavalies nchini Marekani, LeBron James amesema suala la ubaguzi wa rangi haliwezi kuisha nchini Marekani dhidi ya watu weusi.

LeBron amezungumza hayo baada ya watu wasiojulkana kuchora neno Nigga kwenye ukuta wa nyumba yake katika mji wa Los Angeles.

Neno Niga ni neno linalotumiwa na wazungu kuwatusi na kuwakejeli watu weusi nchini Mareknai na duniani kwa ujumla.

LeBron amesema kuwa ubaguzi wa rangi hauwezi kuisha nchini humo hata uwe na pesa kiasi gaini au umaarufa kiasi gaini kuwa mtu mweusi nchini Marekani uwezi kuheshimiwa kabisa na wazungu.

Mchezaji huyo amesema kuwa Wamarekani wenye asili ya Afrika wanapata shida sana kutokana na vitendo hivyo vya ubaguzi kushamili sana licha ya kupigwa marufuku.

LeBron James mwenye umri wa miaka 32 anatambuliwa kama mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi ya NBA, kwa kulipwa kitita cha zaidi ya dola milioni 20 kwa mwaka.

Nyota huyo tokea NBA alitangazwa kuwa ndio mchezaji aliyefunga vikapu vingi katika mchezo wa kikapu nchini Marekani ,na kufanikiwa kuvunja rekodi ya nguli wa mchezo huo, Michael Jordan.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *