Lebo ya MDB yaachana na Young Dee

0
459

Mkurugenzi wa lebo ya Milian Dollar Boys (MDB), Maxlian Rioba amesema kuwa kwasasa lebo hiyo haifanya kazi tena na Young Dee kwa madai kuwa rapa huyo hana nidhamu.

Max Rioba ambaye pia ni producer wiki moja iliyopita alionekana kulalamika katika mitandao ya kijamii akidai rapper huyo amerudi tena katika matumizi ya Madawa ya kulevya.

Kuhusu Young Dee kurudia matumizi ya dawa za kulevya Max amedai kuwa habari hizo na yeye anaziona katika mitandao ya kijamii huku akikiri kutofanya kazi tena na Young Dee kwa madai kuwa hana nidhamu.

Pia Max alidai kama rapper huyo atahitaji msaada wa pesa kutoka kwake ataendelea kumsaidia lakisi sio tena kuwa pamoja kama zamani.

Katika hatua nyingine Max amedai kwa sasa hadhani kama atakuwa na nafasi tena ya kupokea msanii yeyote na kumsimamia kama ilivyo kwa Young Dee kutokana na wasanii kutokuwa na nidhamu baada ya kufanikiwa.

LEAVE A REPLY