Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lameck Ditto amesema kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikosea kutaja jina lake kwa kuwa hahusiki na biashara ya dawa za kulevya wala matumizi ya dawa hizo.

Ditto amesema kuwa hata yeye alisikia jina lake likitajwa kwenye kundi la wasanii ambao wanahitajika kufika leo kituo cha polisi na kusema anadhani kuwa Mkuu wa Mkoa alikosea kutaja jina lake.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa amedaka mtandao unaodaiwa kujihusisha na madawa ya kulevya huku akiwataja wasanii 9 na askari polisi wanaoshutumiwa kujihusisha na mtandao huo.

Miongozi mwa wasanii nao ni Wema Sepetu, T.I.D, Chid Benz, Rachel, Mr. Blue na wengine amao aliwataka wafike kituo kikuu cha polisi leo.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa anataka kumaliza tatizo la madawa ya kulevya katika mkoa huo kwa kudaka mtandao wa wa watumiaji na wauzaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *