Dada wa msanii wa Bongo Fleva, Naj ambaye ni mtangazaji, Lady Naa amesema kwamba familia yao imelibariki penzi la binti yao huyo na mwanamuziki mwenzake, Baraka The Prince kwani wamegundua ndiye mwanaume sahihi kwa mtoto wao.

Lady Naa amesema Naj amewahi kutoka na wanaume kadhaa wakiwemo mastaa wa Bongo Fleva kama Mr Blue na Diamond Platnumz lakini hakuna aliyewahi kuwa na penzi la kweli kwake kwa kumweka kwenye mstari na kumpenda kama ilivyo kwa Baraka.

Dada wa mtangazaji huyo ameongeza kwa kusema wazazi wamemkubali Baraka kwa sababu hanywi pombe wala havuti sigara ni mshauri mzuri wa Naj kwani amefanikiwa kumfanya aache sigara, ishu ambayo ilikuwa inawaumiza sana wazazi wake.

Lady Naa ameongeza kwa kusema kwamba ukiacha figisufigisu za hapa na pale, kwa sasa penzi la Naj na Baraka ndiyo habari ya mjini kufuatia mahaba wanayooneshana popote wanapokuwa.

Baraka The Prince na Naj kwasasa wapo katika mahusiano moto moto ambapo wawili hao mara niyngi uonekana wakiwa pamoja katika safari za ndani na nje ya nchi na hivi sasa wapo nchini Afrika Kusini ambapo Baraka amenda kwa ajili ya kushoot video yake mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *