Lady Madonna akana mipango ya kuasili watoto wengine Malawi

0
589

Staa wa muziki wa Pop wa Marekani, Madonna amekanusha tetesi zinazodai kuwa ametuma maombi ya kuasili mtoto mwingine kutoka nchini Malawi.

Kauli ya Madonna imekuja kufuatia hatua ya msemaji wa serikali ya Malawi kudai kuwa mwanamuziki huyo mkongwe alikuwa kwenye mahakama ya nchini Malawi kuwasilisha maombi ya kuasili mtoto mwingine.

Madonna ambaye tayari ameshaasili watoto wawili kutoka Malawi, yuko barani Afrika kwa kile alichokieleza kuwa ni kutoa misaada ya hisani.

‘Tetesi kuwa niko Afrika kwaajili ya kuasili mtoto mwingine na nimetuma maombi ya kuasili, sio za kweli’.

‘Niko Malawi kuangalia hospitali ya watoto ya Blantyre na kufanya kazi nyingine za hisani na taasisi ya Raising Malawi kisha nitarudi nyumbani’.

Msemaji wa mahakakama ya Malawi, Mlenga Mvula ameyaambia mashirika ya habari kuwa staa huyo amefika mahakama kuu na kuomba kuasili watoto wawili’.

Madonna aliwaasili watoto David Banda mwaka 2006 na Mercy James mwaka 2009.

Madonna ndiye muanzilishi wa taasisi ya kusaidia watoto ya Raising Malawi iliyoanzishwa mwaka 2006.

LEAVE A REPLY