Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura A.K.A Lady Jay Dee anatarajia kuzindua albam yake mpya inayoitwa kwa jina la ‘Woman’ ifikapo Machi 31 mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake Instagram mwanamuziki huyo ameonesha cover inayoonesha tarehe ya kuzinduliwa kwa albam hiyo mpya.

Albam hiyo inatarajiwa kuwa na nyimbo kibao ikiwemo ya nyimbo maarufu Ndindindi, Together Remix na Sawa na Wao na nyingine kibao.

Kwa upande wa meneja wa mwanamuziki huyo Seven Mosha amesema kuwa albam ya mwanamuziki huyo itazinduliwa katika ukumbi wa Bwalo la Jeshi uliopo Lugalo jijini Dar es Salaam.

Meneje huyo wa Rockstars4000 amesema kuwa sababu ya albam hiyo kuzinduliwa katika ukumbi huyo ni ukubwa wa ukumbi pamoja na usalama wa eneo hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *