Staa wa Pop nchini Marekani, Lady Gaga anatarajiwa kuigiza kwenye filamu mpya inayoitwa ‘A Star Is Born’ akiwa kama mmoja wa mastaa kwenye filamu hiyo itakayotoka mwakani.

Filamu hiyo kwa mara ya kwanza ilifanyika mwaka 1954 lakini kwasasa wameamua kuitolea toleo la pili, hapo awali nafasi hiyo ilipangwa kuchukuliwa na Beyonce badala ya Lady Gaga.

Staa wa filamu nchini Marekani,  Bradley Cooper anatarajiwa kuwa muongozaji huku Billy Gerber na Jon Peter wakiwa ndio watayarishaji wakuu wa filamu hiyo.

Lady Gaga: Akiwa jukwaani akiimba wakati wa show yake nchini Marekani.
Lady Gaga: Akiwa jukwaani akiimba wakati wa show yake nchini Marekani.

Pia Lady Gaga anatarajiwa kuandika na kuimba nyimbo mpya kwa ajili ya filamu hiyo inayotarajiwa kuanza kuchezwa kuanzia mwakani.

Lady Gaga anaungana na wanamuziki wengine wa Marekani waliogiza kama vile Mariah Carey na Rihanna ambao pia walipata nafasi kuigiza filamu tofauti nchini Marekani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *