Mwanamuziki na muigizaji nyota wa Marekani, Lady Gaga amefichua siri kwamba yeye na mpenzi wake, Toylor Kinney wametengana kwa muda sasa.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, Lady Gaga amewaomba mashabiki wao wawasaidie ili waweze kurudiana.

 Lady Gaga na Taylor Kinney wamekuwa pamoja kwa miaka mitano lakini uvumi umekuwa ukienea kwamba uchumba wao umeanza kudorora.

Mwanamuziki huyo ameongeza kwa kusema bado wanapendana sana lakini juhudi zao za kutaka kutimiza ndoto zao maishani bado zipo.

Lady Gaga mwenye umri wa miaka 30 alianza mahusiano na Taylor Kinney ambaye ni mwigizaji na mwanamitindo wa Marekani baada ya kukutana wakati wa kuandaa video ya wimbo wa “You and I” mwaka 2011.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *